Tuesday, April 15, 2014

50 CENT HATIANI KWA KUWAIBIA SLEEK AUDIO

50cent_headphones2
RAPPER 50 Cent ameigia katika kesi iliyodumu kwa miaka 3 kati yake na kampuni ya kutengeneza earphone – Bradenton.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.hot97.com, ni kwamba 50 Cent ameamrishwa na mahakama kuilipa kampuni hiyo kupitia kitengo chake Sleek Audio karibia $4.5 million kama fidia ya malipo kwa mwanasheria na $11.7 million kama fidia ya kuvunjika kwa mkataba na kampuni hiyo ambayo ilikuwa wakishirikiana kutengeneza  50 Cent headphones.
50 Cent mwanzoni alituhumiwa kuiba designs za Sleek Audio, ambazo mwanzoni alipewa kwa ajili kuzipitisha kwa ajili ya kuanza kwa uzalishaji wa headphones hizo, lakini baadae 50 aliwageuka Sleek na akaamua kushirikiana na kampuni nyingine kutumia designs alizopewa na kampuni ya Sleek

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI