Saturday, March 22, 2014

PICHA ZA MABAKI YA NDEGE ILIYOPOTEA MALAYSIA

Picha za Satelite ambazo China imesema huenda ni mabaki ya ndege iliyopotea.
CHINA imeanza kuchunguza picha mpya za setilite zinazoonyesha kitu kama mabaki ya ndege katika eneo la kusini mwa bahari ya Hindi.

Maafisa nchini Malaysia wanasema kuwa picha hizo ni muhimu kwa ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea.

Kaimu Waziri wa Usafirishaji Hishammuddin Hussein amesoma taarifa hiyo baada ya kukabidhiwa ambapo amesema kuwa, kuna kitu kama mabaki ya ndege chenye ukubwa wa mita 30 kwa 22 kilichoonekana.

Pia waziri huyo ameongeza kwa kusema kuwa serikali ya China itaendelea kutoa taarifa zaidi hapo baadae.

Ndege MH370 mali ya Shirika la ndege la Malaysia ilipotea baada ya kupoteza mawasiliano ilipoondoka toka Kuala Lumpur kwenda Beijing march 8 mwaka huu ikiwa na abiria 239.
Chanzo: BBC
Baadhi ya picha kabla ya kupotea




0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI