Friday, March 21, 2014

'ANASTASIA GURA' MWAKILISHI PEKEE WA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA 'TOP MODEL' LONDON

MWANAMITINDO Anastazia Gura ambaye ameshawahi kuchaguliwa na mbunifu mkubwa wa mavazi wa Afrika Kusini Olive Clandle kuonesha mavazi yake ameendelea kufanya vizuri katika tasnia hiyo kwa kuwa mmoja wa washiriki wa mashindano ya dunia ya 'Top model' yatakayofanyika huko jijini London nchini Uingereza.
Mwanamitindo huyo ambaye kipindi cha nyuma alishawahi kukaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa anajua kuwa anvyo vigezo vya kutosha kuwa model mzuri, hivyo amepania kufika mbali zaidi.
Kwa kauli hiyo hakuna ubishi kuwa mwadada huyu anajua anachokifanya na anamalengo ya kuifikisha tasnia hii katika nafasi nzuri na hatimaye kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.
Nyota ya mwanadada huyu ilianza kung'ara tangu pale alipochaguliwa mara tu baada ya kuonekana akijaribisha nguo za wabunifu wa kitanzania wanaoshiriki katika onesho la wiki ya mavazi alipoenda nchini Afrika Kusini kwa lengo la kuonesha mavazi ya wabunifu watatu wa kitanzania waliochaguliwa na mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese.
Ndipo alijikuta akichaguliwa kuonesha na mavazi ya mbunifu Olive Clande huku akiwa ndio kwanza anaingia katika tasnia ya uanamitindo angali hajawahi hata kutembea jukwaani.
Hatua hiyo imeonekana kuwashangaza waandishi wa habari wa mitindo na hata wanamitindo wengine waliopo Afrika Kusini kwa kuwa mara zote mbunifu Olive Clande hupendelea kuwatumia wanamitindo wenye majina makubwa.
Na baadaye mbunifu Millen akasema kuwa Anastazia ana vigezo vyote vinavyotakiwa kuwa mwanamitindo kitu pekee kilichomuwezesha kutwaa nafasi hiyo kirahisi.
“Ni kwamba ili uweze kuchaguliwa inatakiwa angalau uwe na vigezo vya kimataifa ili kumwezesha mbunifu kuchagua mtu wa kumuoneshea nguo zake” alisema Millen miaka michache iliyopita.
Mwaka huu Anastazia ameweza kupewa nafasi hiyo kupitia Top Model Tanzania hivyo ataungana na mamodel wenzie siku si chache kwaajili ya kushiriki katika mashindano hayo yanayojumuisha washiriki toka maeneo mengi duniani.

Mwanamitindo huyu ambae matunda yake yameanza kuonekana mapema Anastazia Gura akitengenezwa nywele kabla ya kupanda jukwaani.



0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI