Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu masuala ya Muungano katika ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) mjini Dodoma ljana.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala ya Muungano katika ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) mjini Dodomajana
Picha na Magreth Kinabo – MAELEZO
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema kwamba Muungano wa Tanzania utakuwepo na utaendelea kudumu, hivyo hakuna mtu atakayeweza kuuhujumu au kuuvunja kwa maslahi yake binafsi.
Aidha Makamu huyo wa Rais wa Zanzibar amesema kauli iliyotolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar , Maalim Seif Sharrif Hamad hivi karibuni kuwa Wanzanzibari wote wanataka Muungano wa Mkataba si kauli ya kweli kwa kuwa hakuwahi kuzungumza na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wala wananchi, hivyo wananchi wasitishike.
Kauli hiyo imetolewa na Balozi Seif wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala ya Muungano na mchakato wa Katiba Mpya katika ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) mjini Dodoma jana.
“Wanzanzibari wengi wanauthamini Muungano tungependa kuuendeleza na kuihimarisha kwa maslahi ya pande zote za Muungano.
“ Katika mchakato huu,tumeshuhudia baadhi ya wanasiasa kuonesha dhahiri ni zao za kutaka kuvuja Muungano kutokana na kauli zao . Kauli nyingi zinatolewa zenye kuchonganisha wananchi wa pande mbili za Mujungano, alisema Balozi Seif.
Alisema kwa mfano ,kauli za kusema Wazanzibari wote hawataki Muungano wanataka Mkataba “ Naomba kuuliza ni Wazanzibari gani hao wanaosemea mbona sisi hapa pia ni Wazanzibari na hatuna msimamo huo wa mkataba? alihoji Balozi Seif.
Akifafanua swali lililoulizwa na mwandishi wa habari kuwa kauli aliyoitoa Maalim Sief kuwa ni ya Serikali, Balozi Iddi alisema si kweli kuwa kauli hiyo ni ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“ Maalim Seif kasema kama Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF) wala si kwa niaba ya Serikali. Hakusema kama Makamu wa Pili wa Rais,” alisisitiza Balozi Seif . Hivyo wananchi watambue kauli hiyo ni ya uongo na hana uwezo wa kusema lolote.
Aliwataka wananchi wa Zanzibar watambue kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko macho na yeyote atakayefanya fujo atashughulikiwa kikamilifu.
Alisema Muungano una faida kwa Wazanzibari kuliko Watanzania Bara katika umoja na kupanua wigo mpana wa matumizi ya ardhi,biashara na ajira.
Akizungumzia kuhusu mchakato wa Katiba Mpya alisema unakabiliwa na changamoto za kukosekana kwa uvumilivu miongoni wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Bunge hilo kutawaliwa na hisia za kisiasa badala ya maslahi ya Taifa na kuna vikundi vya wachache wasiotaka mchakato huu uendelee kutokana na utashi wa kisiasa.
“ Vitendo vya uvunjifu wa amani kila siku ili Bunge liahirishwe kwa sababu tu za kibinafsi za baadhi ya wanasiasa si jambo jema hasa kwa kuwa kodi ya Watanzania inapotea bila ya kufanya kazi iliyokusudiwa kuifanya na sisi waheshimiwa wajumbe, “ alisema huku akisisitiza kuwa hali hiyo haitaweza kustahimiliwa.
Balozi Sief alisema wako katika Bunge hilo kwa kutetea maslahi ya Watanzania na sio mtu binafsi.
Aliwataka viongozi hao kuwa mfano mwema wa matendo mazuri mbel e ya jamii ya Watanzania na kujenga utamaduni wa kuvumiliana na kustahimiliana na kuheshimiana ili lengo la Katiba Mpya liweze kutimia kwa maslahi ya taifa na Watanzania .
Akifafanua kuhusu makundi yaliyoundwa katika mchakato huo ambayo baadhi yao kuwa ni Tanzania Kwanza na Ukawa kuwa si rasmi bali yameundwa kwa utashi
0 comments:
Post a Comment