Sunday, March 23, 2014

KIM KADARSHIAN NA KANYE WEST KATIKA JARIDA LA VOGUE

IMEELEZWA kuwa ni muda mrefu sasa umepita mwanamuziki maarufu nchini marekani katika muziki wa mitindo ya kufokafoka ama Hip hop, Kanye West amekuwa akitamani kuwepo katika kurasa za mbele za jarida moja maarufu sana nchini marekani la Vogue.
Ndoto ama hamu hiyo hivi karibuni ilitimia baada ya kupewa hiyo nafasi na Annie Leibovitz katika ukurasa huo wa mbele ambapo jarida hilo litatoka mwezi wa nne.
Picha iliyowekwa imemuonesha Kim Kardashian akiwa amevalia gauni la harusi akiwa ameshikiliwa na Kanye West, ambapo baada ya kuipata picha hiyo mwanadada huyo alitupia katika ukurasa wake wa twitter na Instagram na kusema Asanteni "Hii ni ndoto iliyogeuka kuwa ya kweli" naye Kanye akaandika "Asanteni @Voguemagazine" katika ukurasa wake wa twitter.
West amesema alikuwa anaamini Kardashian ana kila kitu cha kumuwezesha kuwa katika ukurasa wa mbele wa jarida la Vogue alipokuwa akihojiwa na Ryan Seacrest katika kipindi cha redio oktoba ya mwaka jana. Akasema:
"Haiwezekani Kim akakosa kuwa katika jarida hilo kwani ana kila kigezo" akaongeza kuwa "Kardashian ana mvuto hata kumzidi mke wa rais wa marekani Michelle Obama katika machaguo ya nguo anayoyafanya.
Hata hivyo katika jarida hilo litakalotoka March 31, mhariri mkuu wa jarida hilo amesema lilikuwa ni wazo lao kumshirikisha mwadada huyo na si kwamba walifanya kile  ambacho Kanye alikisema juu ya mwadada huyo kuwepo katika jarida hilo.
"Yaweza kuwa magazeti mengi yameandika kuwa Kanye West ameniomba kuwa nimuweke, lakini ukweli ni kwamba hakufanya hivyo"
Kwa sasa wapenzi hao wamebarikiwa mtoto mmoja ambaye ana miezi 9 na wamempa jina la North.


0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI