MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), juzi imevifungia kufanya biashara ya mafuta ya jamii ya petroli vituo sita katika wilaya za Chunya, Mbozi na Momba, mkoani Mbeya, kutokana na kukiuka masharti ya biashara.
Mkaguzi wa bidhaa za petroli wa EWURA Mhandisi Raphael Nyamamu, amesema vituo viwili hiolkatika wilaya ya Chunya vimefungiwa kufanya biashara kwa sababu havina leseni ya biashara na kwa hiyo vilikuwa vinaendesha biashara hiyo kinyume cha sheria.
Katika wilaya ya Mbozi, kituo kimoja kimefungwa kwa kukosa leseni ya biashara, wakati katika Wilaya ya Momba, kwenye mpaka wa Tunduma, jumla ya vituo vitatu vimefungwa kwa makosa ya kukosa leseni ya biashara na kimoja kwa kuuza mafuta yasiyokidhi viwango.
Hatua hii inakuja wiki moja toka EWURA ikifungie kituo cha Gapco Service Station Mbeya, kilichopo katikati ya jiji, baada ya mamlaka hiyo kubaini ubora hafifu wa mafuta yaliyokuwa yanauzwa kituoni hapo.
Mamlaka hiyo imevifungia vituo vingine viwili vya Lake Oil kilichopo Kyela na TSN cha Kiwira kwa kosa la kuendesha biashara pasipo na leseni ya EWURA.
Kwa mujibu wa Mhandisi Nyamamu, vituo vya Gapco Mbeya na Oil ComTunduma vimekuwa vituo pekee kupatikana na mafuta yasiyokidhi viwango vya ubora kati ya vituo 26 vilivyokaguliwa mkoani Mbeya. ujumla, zoezi la ukaguzi mkoa wa Mbeya hadi sasa limebaini kuwepo kwa vituo viwili tu vyenye mafuta yasiyo na ubora unaotakiwa...kimoja ni cha Gapco Mbeya alisema Mhandisi Nyamamu.
Mhandisi huyo alisema timu ya wataalam wa EWURA ipo mkoani Mbeya ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa kushtukiza kwa kanda ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo mkoa wa Mbeya umekuwa ya kwanza kukaguliwa, na kwamba matokeo hadi sasa yanaonyesha soko lina mafuta yenye ubora mzuri, licha ya vituo vya Gapco na Oil Com.
0 comments:
Post a Comment