Wednesday, March 26, 2014

BENKI YA NBC YAKABIDHI ZAWADI YA GARI KWA MSHINDI WA SHINDANO LA WEKA UPEWE

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Bi Mzinga Melu (kushoto) akikabidhi zawadi ya gari jipya aina ya Suzuki Swift kwa Bi. Mary Malifedha Popote mkazi wa Kigoma, aliyeibuka mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe iliyokuwa ikiendeshwa na NBC. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki hiyo, Mussa Jallow, Mkuu wa Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bi. Mwinda Kiula Mfugale. Gari hilo lina thamani ya dola za kimarekani 17,000. 
Mshindi wa gari wa promosheni ya Weka Upewe ya NBC, Mary Malifedha Popote akifungua mlango wa gari lake baada ya kukabidhiwa. Nyuma yake ni Mkuu wa Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bi. Mzinga Melu.
Mshindi wa gari wa promosheni ya Weka Upewe ya NBC, Mary Malifedha Popote akiwasha gari lake jipya aina ya Suzuki Swift tayari kwa safari ya kwenda Kigoma. 

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI