Monday, December 3, 2012

KINGALAME WA TBC1 AOLEWA!


Na Erick Evarist
HAYAWI hayawi sasa yamekuwa! Hatimaye mtangazaji maarufu wa Televisheni ya Taifa (TBC1), Grace Kingalame amefunga ndoa na Mhariri wa Michezo wa Gazeti la Jambo Leo, Julius Kihampa.
Julius Kihampa na mkewe Grace Kingalame.
Ndoa ya wawili hao ilifungwa Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Albano, Posta, jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na harusi ya kukata na shoka iliyochukua nafasi kwenye Ukumbi wa PJ, Kinondoni, Dar ambapo ndugu, jamaa na marafiki walikuwepo kujirusha mwanzo mwisho.

Kabla ya ndoa Jumamosi, Desemba 29, mwaka huu familia ya Grace iliangusha shughuli ya kumuaga (send off) mtangazaji huyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mwenge Social, Dar es Salaam.
Wawili hao wakichukuwa msosi.
Grace akimsaka mumewe.
Bibi harusi akiwa na wapambe wake.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI