Gari aina ya scania lenye Cabin no. T 840 BST likiwa na trailer no. T 566 BNQ lililogongwa kwa nyuma na toyota RAV 4 T 770 BMP na kusababisha vifo vya wanafamilia hao.
Habari kwa hisani ya francis godwin, Picha na Misanjo Livigha
AJALI mbaya imetokea mkoani Iringa mchana wa leo na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani mmoja.Ajali hiyo imetokea katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye kizuizi cha barabara cha mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa - Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane mchana.
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 yenye namba za usajili T 770 BMP kulipalamia lori lenye tela kwa nyuma.
Huku chanzo kikitajwa kuwa ni kuendesha kwa mwendo kasi wa dereva wa gari dogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke na kushindwa kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma. ambapo gari hiyo ndogo ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya.
Katika ajali hiyo wanafamilia wote watano akiwemo baba na mama wa watoto wawili pamoja na mfanyakazi wa ndani wamefariki dunia papo hapo na maiti zote kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
Majina ya waliopoteza maisha ni pamoja na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ndiye aliyekuwa dereva wa gari hilo na baba wa familia hiyo, mkewe Grace Mwaiteleke, mtoto Kelvin Mwaiteleke(2), Happy Mwandike na mfanyakazi wao wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel, huku aliyenusurika katika ajali hiyo ni mmoja na amekimbizwa Hospitali ya mkoa wa Iringa kwa matibabu.
0 comments:
Post a Comment