NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Sunday, October 28, 2012

MAMA WA MTOTO ALIYEKOJOLEA MSAAFU AOMBA RADHI.



HATIMAYE mama wa mtoto aliyekojolea msaafu na baadae kuzua gumzo ndani ya waumini wa dini ya kiislam na wakristo ambalo limepelekea mali nyingi ikiwemo kuteketezwa kwa makanisa huko Mbagala jijini Dar es salaam, watu kupoteza uhai, na wengine wakiwa hospitalini bado wakijiuguza majeraha.

Inaripotiwa kuwa mama huyo Bi. Teresia Josephat siku ya jumamosi katika mahojiano na mwandishi wa gazeti amesema kuwa hajawahi tegemea kama kitendo hicho kingefanywa na mwanae Emmanuel Josephat (14) kwani alimkuza katika malezi na maadili mema tu.

Mda mrefu kidogo umepita, katika mabishano ya rika kati ya kijana huyo na wenzake, ndipo ikafikia kijana huyo kukidhihaki kitabu kitukufu cha kuruani  kwa madai kwamba angelifanywa hivyo angeweza kugeuka mnyam

Mtandao huu UNAPINGA na KULAANI kitendo cha mtu wa dini fulani kumdharau au kumuona hana haki mtu wa dini nyingine, wote tunamwabudu Mungu mmoja hivyo yatupasa kujitakasa kwa kutodharauliana kiimani.

NSSF: "HATUIPINGI FAO LA KUJITOA''

Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii NSSF Dkt. Ramadhan K Dau akijibu maswali yaliyoulizwa na Wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya POAC (hawapo pichani).
Katika Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mahesabu za Mashirika ya UMMA (POAC) mnamo tarehe 24/10/2012 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhani K. Dau akijibu maswali ya Waheshimiwa Wabunge alitoa maelezo ya msingi kuhusu umuhimu na dhana kamili ya Hifadhi ya Jamii.

Katika maelezo hayo alifafanua kuhusu madhara ya kujitoa kwenye mfuko kwa mwanachama aliye na uwezo wa kuendelea na kazi, na alisisitiza kuwa madhara ni kwa Mwanachama zaidi kuliko kwa Mfuko. Dkt.Dau alifafanua kuwa uamuzi wa kusitisha kwa Mafao ya kujitoa hauna uhusiano wowote na hali ya sasa ya kifedha ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Dkt. Dau aliieleza Kamati ya Bunge kuwa hali ya kifedha ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii hupimwa kwa kufanya Actuarial Valuation. Kwa upande wa NSSF zoezi hilo limefanywa mwaka 2009 na Kampuni kutoka Canada iliyoteuliwa na ILO na mwaka 2010 na Kampuni kutoka Afrika Kusini iliyoteuliwa na SSRA.

Matokeo yameonyesha kuwa NSSF HAINA MATATIZO YA KIFEDHA kwa sababu ina uwezo wa kuwalipa Wanachama wake na kulipia gharama za uendeshaji kwa kipindi cha miaka 50 ijayo bila kutetereka.

Dkt. Dau alifafanua zaidi kuhusu kutokuwepo kwa mafao ya kujitoa katika mfumo mzima wa Pensheni ulimwenguni kwa muongozo wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) namba 102 wa mwaka 1952 [The ILO Social Security (Minimum Standards) Convention, 1952 No. 102] ambao ndio unatoa maelekezo ya jumla kuhusu Sekta ya Hifadhi ya Jamii ulimwenguni kote.

Katika Muongozo huu ILO imetamka wazi kuwa kuna aina tisa (9) za mafao yanayotolewa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na katika hayo hakuna mafao ya kujitoa. HITIMISHO Tunapenda kuwataarifu Wanachama na Wananchi kwa ujumla kuwa majibu haya ndio yaliyotolewa katika Kamati ya Bunge.

Taarifa zilizotolewa na baadhi ya Vyombo vya Habari kuwa “Mkurugenzi Mkuu wa NSSF apinga Mafao ya Kujitoa” zimetolewa nje ya maudhui yaani “Out of Context” Suala la Mafao ya kujitoa (Withdrawal Benefit) linashughulikiwa na Serikali na iwapo itaamuliwa na Bunge kurudisha mafao hayo,

NSSF HAINA PINGAMIZI na uamuzi huo na italipa mafao hayo bila wasiwasi wowote kwani ina uwezo mkubwa wa kifedha.

IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO - NSSF

Friday, October 26, 2012

EID MUBARAK JAMANI EH!!!


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Viongozi wengine wakijumuika na waislamu na wananchi katika  swala ya EID el Hajj katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo

Uongozi wa mtandao huu wa ulimwenguwahabari.blogspot.com unawatakia waislamu wote Eid Mubarak popote pale walipo duniani.

Kupitia mtandao huu wa ULIMWENGU WA HABARI pia tunapenda kuwaasa ndugu zetu waislamu pamoja na wale wa kikristo kushikamana katika kuiendeleza amani ambayo hayati Mwl. J.K Nyerere baba wa taifa hili na mzee mwenzie Abeid Karume walituachia kama msingi wa umoja na Usawa kwa wote.

Pia viongozi hao walisisitiza kuwa watanzania wote ni ndugu, hivyo kwa wale waliokuwa na uwezo ni vyema basi wakashiriki chakula cha pamoja na wale ambao katika siku hii ya leo hawajajaaliwa kwani kwa kufanya hivyo atapata baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu!!!

                                                                   EID-MUBARAK!!
                                                          ULIMWENGU WA HABARI

Wednesday, October 24, 2012

WASOMI VYUO VIKUU: ''VYOMBO VYA HABARI VIIHAMASISHE JAMII KUACHANA NA RUSHWA''

VYOMBO vya habari vimepewa jukumu la kuelimisha kutaarifu na kuhamasisha Umma katika masuala mbalimbali yaliyopo katika jamii.

Kwa kuyatambua hayo mwandishi wa mtandao huu anapata fursa ya kuzungumza na Mhadhiri Msaidizi wa chuo Kikuu cha Tumaini - Iringa bw. Simon Berege ambaye anazungumzia ni jinsi vyombo vya habari vina wajibu wa kupambana na rushwa.

Anaanza kwa kusema;
''Tunategemea kwamba vyombo vya habari vifanye kazi zaidi, vivuke mipaka ya kuhabarisha, kuburudisha, kushawishi na hatimaye vijikite katika majuku maalum, ambayo ni kupambana na rushwa kwaajili ya maslahi ya taifa''

Bw. Simon akaenda mbali zaidi kwa kuongelea suala  ushawishi wa vyombo vya habari kuwa ni mkubwa sana katika jamii, hivyo vyombo vya habari havinabudi kuishawishi jamii kuepukana na masuala mazima ya vitendo vya rushwa.

Bw. Simon Berege, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Tumaini - Iringa akiongea na mwandishi wa habari kuhusiana na masuala ya rushwa.
kabla ya kuondoka katika eneo hilo mwandishi wa mtandao huu anapata fursa pia ya kuzungumza na Agnes Shija ambae ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu - Tumaini cha Dar es salaam, nae anaeleza umuhimu wa kukemea rushwa kupitia vyombo vya habari.

''Hali ya vyombo vya habari kwa sasa katika mchakato mzima wa kupambana na rushwa kwakweli ni wa kiwango cha juu, kwasababu vyombo hivyo vimejitahidi kufichua kila matendo ya rushwa yanapotokea lakini pia vimeonesha hasara zinazojitokeza pale ambapo matukio hayo yanapojitokeza kwa mfano masuala ya EPA, ubadhilifu wa ardhi n.k kitu ambacho kimewawezesha wananchi kufahamu hali halisi na chanzo cha matatizo yao, lakini pia kuwaonesha njia kuwa wanahaki ya kufuatilia kisheria na kuyapeleka matatizo yao katika sehemu husika zinazoshughulikia masuala ya rushwa'' alisema Bi. Agnes Shija.
Bi. Agnes Shija, Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini - Dar es salaam akiongea na mwandishi wetu juu ya umuhimu wa vyombo vya habari kupambana na rushwa katika jamii. 


Rushwa bado imekuwa kikwazo katika nchi zinazoendelea, hivyo hatuna budi kama wanajamii kuungana kwa pamoja mimi, wewe na yule kuipinga na kupingana kabisa na vitendo vya utoaji na upokeaji rushwa ya aina yeyote ile; hapa nikimaanisha rushwa ya ngono, fedha mali n.k

Kwa nguvu moja wananchi tuipinge RUSHWA!
k

Sunday, October 21, 2012

DKT. HARISSON MWAKYEMBE KUSHGHULIKIA MAPENDEKEZO YA KAMATI ILIYOTEULIWA KUCHUNGUZA MADUDU KATIKA BANDARI YA DSM.

Waziri Mwakyembe kulia akipokea ripoti ya uchunguzi katika bandari ya DSM, kulia ni mwenyekiti wa kamati hiyo Bernard Mbakileki {Picha na father kidevu}
  Na Deogratius Maro, Hilali Ruhundwa
WAZIRI wa uchukuzi Dkt Harison Mwakyembe amesema, hadi kufikia disemba mwaka huu atahakikisha wizara yake inatekezeleza mambo  yaliyopendekezwa kwenye  kamati ya kuchunguza utendaji  kazi wa  mamlaka ya  ya bandari nchini TPA ili kutoa sura mpya ya  kiutendaji 
Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara  baada ya kuipokea ripoti ya kamati hiyo ya watu saba aliyoiteuwa agosti 27 mwaka huu kuchunguza masuala mbalimbali katika bandari ya Dar es salaam
Amesema mamlaka ya bandari Tanzania TPA ni miongoni mwa bandari kubwa elfu 36 barani afrika ambapo licha ya ukubwa na ukongwe huo utendaji wake umekuwa ni mbovu na hivyo kusababisha wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya nchi kuancha kutumia bandari hiyo na badala yake kutumia bandari ya Mombasa.

Bandari ya Dar es salaam

 Dkt . Mwakyembe amesema bandari hiyo imekithiri ubabaishaji, wizi, pamoja na gharama za kutolea mizigo  na ushushaji kutoongezeka hali inayochangia wafanyabishara wengi kutotumia bandari hiyo.
Kitendo cha kuwasimamisha kazi baadhi ya watendaji katika mamlaka hiyo kimechangia kurudisha utendaji kazi na imani kwa wafanyabishara wakubwa wa ndani na nje nchi ambapo baadhi yao tayari wameanza kujitokeza kwa ajili ya kufanya kazi na mamlaka hiyo.

POLISI ZANZIBAR WAKANUSHA TAARIFA ZA KUMTEKA SHEIKH FARID HADI AHMED

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzbar Mussa Ali Mussa
JESHI la Polisi Zanzibar limesema halihusiki kwa kupotea kwa kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Farid Had Ahmed ambaye alionekana juzi usiku majira ya saa 2.15 na kuonana na familia yake hapo Mbuyuni.

Akizungumza na waandishi wa habari hapo Ziwani Mjini, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa alisema jeshi lake halihusiki kwa namna yoyote ya kuchukuliwa kwa Shekh Farid katika mazingira ya kutatanisha.

“Jeshi la Polisi linakanusha kuhusika katika sakata la kutekwa kwa kiongozi wa Uamsho... tunamhoji kujua ukweli katika tukio hilo zima,” alisema Mussa.

Shekhe Farid alihojiwa na Jeshi la Polisi baada ya kujisalimisha kufuatia kuwepo kwa taarifa za kupotea katika mazingira ya kutatanisha na kupelekea kuibuka kwa fujo na vurugu kutoka kwa wafuasi wake.

Hata hivyo, haijafahamika kama Jeshi la Polisi litachukuwa hatua gani baada ya kumaliza kazi za kufanya mahojiano na kiongozi huyo wa Uamsho, ambapo katika siku nne ya kutoweka kwake matukio mbalimbali yaliibuka ikiwemo kifo cha polisi mmoja na wananchi kufanya vitendo vya uporaji wa mali.

Akizungumza na waandishi wa habari hapo Mbuyuni, Farid alisema hakutekwa, lakini alichukuliwa na Jeshi la Polisi na vikosi vya Usalama wa Taifa wakimhoji kuhusu harakati zake za kuitetea Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano.

Ripoti iliyoandaliwa na Deogratius!

Saturday, October 20, 2012

SMZ YAPIGA MARUFUKU URUSHAJI WA MATANGAZO YA KIKUNDI CHA UAMSHO ZANZIBAR!

Source: Wavuti.com

ZILIZOSOMWA ZAIDI