Wednesday, November 9, 2016

SIMBA YAKUBALI KIPIGO CHA GOLI 2-1 KUTOKA KWA TANZANIA PRISONS

MCHEZO wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Tanzania Prisons uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, umemalizika kwa wekundu hao kukubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya maafande hao.
Timu ya Simba ilianza kupata bao lake katika dakika ya 43 kupitia winga wake Jamal Mnyate akiunganisha krosi nzuri kutoka kwa Shiza Kichuya.
Katika kipindi cha pili dakika ya 48 Prisons walipata bao la kusawazisha kupitia Victor Hangaya baada ya kuunganisha mpira wa krosi ya Kimenya. 
Prisons walipata bao la pili, mfungaji akiwa yuleyule Hangaya na kufanya mchezo huo kumalizika wa 2-1.
Katika hatua nyingine timu ya Azam imeiadhibu Mwadui FC 4-1.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI