KWENYE mahojiano wiki hii rapa Remy Ma aliyesikika sana kupitia wimbo wa #AllTheWayUp na Fat Joe amesema hapakuwa na kazi iliyofanyika kati yake na Nicki Minaj.
Remy anasema “Nilipotoka jela Minaj alinipigia simu na tukapanga colabo ila alisema iwe siri na baadae yeye ndio akaivujisha hio siri, kama alitaka wimbo na Foxy Brown angefanya mapema hata bila mimi, watu wanajua tuna vipaji na wanataka kuona vikiwa pamoja ila kwenye maongezi yetu nilimuambia kuwa watu watatugombanisha na ndio kinachotokea sasa ila sina tima ya kumdiss mtu bila sababu”
Wiki mbili zilizopita Nicki Minaj alisema kuna colabo na Remy Ma na imetayarishwa na Diplo.
Remy pia anasema ni muda wasanii wa kike waache majigambo yao ili tufanye kazi pamoja kama wakina Drake, Rick Ross, na French Montana wakifanya colabo inakuwa kubwa sana.
0 comments:
Post a Comment