Saturday, June 28, 2014

JAY Z & BEYONCE WAME-SHARE VIDEO YA NDOA YAO KATIKA UZINDUZI WA ON THE RUN TOUR, MIAMI

JAY Z na na wife wake BEYONCE wameamua kuwaonesha mashabiki wao kuwa bado ndoa yao iko vizuri na inazidi kuwa ngangari kwa kuwaonesha vipande vya video yao ya ndoa ambavyo havikuwahi kuoneshwa hapo kabla katika vituo vya runinga nchini Marekani.
Tukio hilo limefanyika katika uzinduzi wa music tour yao waliyoipa jina la 'On the Run Tour, OTR' ambapo walicheza takribani nyimbo zao 42 zinazohit ulimwenguni na kuweka video hiyo nzuri na kuvutia kama backdrop yao wakiwa wanapafomu.
Wawili hao walioana kwa siri mwezi April 2008 baada ya kuwa wapenzi kwa miaka 6 na wamekuwa wasiri sana linapokuja suala la mapenzi na ndoa yao, lakini wameamua kucheza vipande hivyo vya video na kuonyesha baadhi ya clip za mtoto wao Blu Ivy akiwa mdogo kabisa.
Angalia vipande hivyo hapa chini….!!!
Enjoooooy.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI