Saturday, November 5, 2016

NDOA IMENIONGEZEA HESHIMA NA UMAKINI KWENYE MAISHA YANGU – TUNDA MAN

Tunda Man akiwa na familia yake
IKIWA ni wiki tatu toka msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man aingie kwenye maisha ya ndoa, amefunguka na kuzungumzia jinsi maisha ya ndoa yalivyobadili maisha yake.
Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Tunda amesema ndoa imemfanya kuwa makini zaidi ya maisha yake kwa kuwa tayari ana familia ambayo inamtegemea.
“Maisha yamebadilika sana, heshima imeongezeka, nimekuwa makini zaidi kwa sababu kuna watu ambao wapo nyuma yangu,” alisema Tunda Man. “Pia ndoa ni nusu ya dini ya uislam. Kwa hiyo naweza kusema haya ni maisha mapya ya Tunda Man ambayo yamejaa baraka ndani yake,”
Pia muimbaji amesema ndoa yake haitamzuia kufanya shughuli zake za muziki ambazo zinamuendeshea maisha yake.
Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo ‘Mama Kijacho’ anajipanga kuachia kazi mpya hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI