Friday, November 4, 2016

MSANII YEMI ALADE AMSIFIA NANDY

MSANII wa Nigeria anayetarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta Jumamosi hii ya Novemba 5, Yemi Alade amemsifia Nandy kwa kudai kuwa alitabiri atakuwa msanii mkubwa.
Akiongea mbele ya waandishi wa habari Ijumaa hii wakati wa kuwatambulisha wasanii watakao washa moto kwenye jukwaa la tamasha hilo, Yemi Alade ameisifia video mpya ya msanii huyo ‘Nagusagusa’ na kusema kuwa alijua tangu mwanzo muimbaji huyo atakuwa ni msanii mkubwa kwa kuwa alishawahi kumuona kwenye mashindano ya kutafuta vipaji ya Afrika yaliyofanyika nchini Nigeria.
Nandy ni msanii mmoja wapo aliyechaguliwa kuwasha moto kwenye tamasha hilo, wasanii wengine ni pamoja na Weusi, Maua Sama, Navy Kenzo, Alikiba, Mr Blue, Rayvanny, Darassa, Jay Moe, Barakah The Prince, Bill Nas, Fid Q, Belle 9 na wengine.
Tekno, Yemi Alade na baadhi ya wasanii wengine wa Bongo Fleva wakiongea na waandishi wa habari
Wasanii wengine kutoka nje ya Tanzania ambao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye jukwaa hilo ni pamoja na Tekno (Nigeria) na Chameleon (Uganda).

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI