Tuesday, November 15, 2016

MISS TANZANIA 2016 DIANA EDWARD ADAIWA KUIKACHA KAMPUNI ILIYOMTOA

KAMPUNI ya filamu nchini ya Timamu Effect iliyomtoa mshindi wa shindano la Miss Tanzania 2016, Diana Edward imedai kutelekezwa na mrembo huyo.
Wakiongea na kipindi cha Kubamba cha Times FM, meneja wa kampuni hiyo Timoth Conrad na meneja vipaji, Mama Ashura wamesema kuwa mrembo huyo hakuwa na wazo la urembo na wao ndio waliomshauri na kumuandaa.
“Alikuja kama muigizaji na mtangazaji ila sisi tukagundua anaweza kuwa Miss tukaanza kumjenga. Tulimuandaa akashinda Miss Ubungo, Miss Kinondoni ila baada ya kushinda taji la Tanzania nzima hatukumbuki. Mimi ninachomshauri tu akumbuke alipotoka hatuna haja na zawadi ila heshima ya alipotokea,” amesema meneja Mama Ashura.
Katika hatua nyingine uongozi wa kampuni hiyo umedai kuwa unazo nyaraka zote za mkataba aliosaini mrembo huyo na kampuni hiyo ya Timamu lakini kwa sasa bado haijaamua kwenda mahakamani.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI