Kutana na Timoth Conrad Kachumia
‘Tico’, mtanzania ambaye nguvu zake, akili yake na utundu wake siku
zote ameuelekeza kwenye utengenezaji wa filamu za Kitanzania akiwa kama
‘muongozaji na muandaaji’
Timoth ameipa Tanzania headlines kwenye tuzo za SILICON VALLEY AFRICAN FILM FESTIVAL ambazo zimekua zikifanyika kila mwaka California, Marekani kwa kushinda tuzo moja ya ‘Achievement in Narrative Feature Film‘ iliyokuwa ikiwaniwa na nchi 9 za Afrika.
Kwenye exclusive interview na reporter wako Millard Ayo aliyeko hapa Marekani, Timoth amesema ‘kwenye hicho kipengele nilikua nashindana na Ghana, South Africa, Nigeria, huu ni wakati wa Watanzania kuamka na kufanya kazi nyingi nzuri zaidi, huu ushindi sio kitu kidogo upinzani ulikua mkubwa’
‘Tumekubalika sana… hii filamu yangu
inawazungumzia watoto watatu waliokua wakitafutwa na viumbe vingine
kutoka sayari nyingine, sio stori ya kweli ila ni ya kufikirika… ni
stori ambayo niliiandika mwenyewe’ – Timoth
#Milladayo.com






0 comments:
Post a Comment