Sunday, September 13, 2015

UVCCM WAMVAA MAALIM SEIF WAMTAKA AACHE KUBEZA MAFANIKIO YA SUK

UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi umemtaka Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad kuacha kuupotosha umma na kubeza mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya umoja wa kitaifa inayoongozwa na Rais Dk Ali Mohamed Shein.

Imemtaka awe muungwana na msemakweli kuhusu mafanikio yaliyofikiwa ingawa yeye binafsi na chama chake wamekuwa wakichukia hilo.
Pia imemtaka kutoudanganya umma kwa madai atamudu kuwapa ajira vijana Wanzibari wote katika kipindi kifupi endapo atachaguliwa kuwa Rais.

Taarifa ya UVCCM kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wake, Shaka Hamdu Shaka jana ilisema Seif ni kiongozi kigeugeu ambaye hupenda kuudanganya umma na kusema serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar imeshindwa kufikia yake maendeleo yake katika kipindi tangu iundwe miaka mitano iliopita .

Shaka alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)  huongozwa kwa pamoja kati ya CUF na CCM hivyo madai anayotoa Seif hivi sasa yanalenga kuupotosha umma na kuficha ukweli.

“Nichukue nafasi hii kuwaeleza wananchi  Serikali ya Umoja wa Kitaifa chini ya  Dk.  Shein huongozwa kwa pamoja  kisera  na mawaziri toka CCM na CUF seif akiwa makamu wa kwanza wa Rais. Uamuzi, ushauri na utekelezaji sera na pamoja na mikakati hupitishwa na kutekelezwa katika Baraza la Mapinduzi ambalo Seif pia hushiriki na kushauri ” alisema shaka.

Kwa mujibu wa Shaka, serikali ya CCM imetekeleza majukumu yake kazi kwa Wazanzibari kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo ya kisekta ikiwemo kukuza uchumi, afya , miundombinu ,  utalii na elimu.

Alisema serikali ya CCM chini ya Dk. Shein imepandisha bei ya karafuu zao ambalo ni tegemeo kubwa la kiuchumi kwa Wanzibari wengi.

Kaimu Katibu Mkuu huyo aliwaomba Wazanzibari kuwa makini na wanasiasa aina ya Maalim Seif kwa wamekuwa na ndimi mbili zinazomfanya ashindwe kusifu mema hata pale ukweli unapodhihiri.

“Seif akumbuke hisani pia awe na shukran  bila  kubeza mafanikio ya  SUK  ati imeshindwa kufikia malengo yake, huo ni uongo na uzushi wa  Maalim Seif ambaye amekuwa akisaka  urais wa Zanzibar bila mafanikio tangu mwaka 1984 alipoanza  kushindana  na marehemu mzee idris abdul wakil huku kushindwa mara nne kufikia lengo lake  nje ya ccm .

“Hivi kwa akili ya kawaida mtu unayeshirikiana naye katika utekelezaji na uendeshaji serikali mwenye wadhifa wa Makamu wa Kwanza wa Rais kama  Maalim Seif ndani ya SUK, anawezeje kuwa mdanganyifu na kuyapa kisogo mafanikio yaliyopatikana chini ya Dk. Shein.

“Ikumbukwe  serilali inayoongozwa na Dk. Shein ndiyo iliyopandisha bei ya zao la karafuu, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zinanazofika hadi katika kijiji ambacho Maalim Seif anadai amezaliwa huko Mtambwe ikiwemo kuondoa tatizo la usafiri wa Pemba na Unguja baada ya serikali kununua meli ya kisiasa ambayo iko njini kufika Zanzibar wakati wowote huku uchumi ukikua kwa kasi ya asilimia 7,” alihoji Shaka.

Mbali na hayo, Shaka alisema chini ya uongozi wa Dk. Shein serikali yake  imefanikiwa kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma mara tatu katika kipindi cha miaka mitano jambo ambalo alisema ni mafanikio makubwa katika kuimarisha huduma za maendeleo ya jamii.

“Serikali humudu kumsafirisha Maalim Seif nje ya nchi mara tatu kwa ajili ya kupata matibabu  tangu afya yake ilipoanza kuzorota. Bila uchumi kuimarika smz  isingeweza kubeba gharama hizo” alisema  shaka.

Aidha Uvccm  imemuonya aliyekuwa Waziri katika  SMZ Mansour Yussuf Himid kuacha mara moja kutumia msamiati wa mapinduzi daima katika jukwaa la cuf kwasababu mapinduzi hayo hayana asili na cuf wala hizbu iliokuwa ikipingana na ASP  kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka  1964.

"Tunamtaka Mansour aache kutumia neno mapinduzi katika mikutano ya cuf, Mapinduzi ya zbr hayana mnasaba wala uhusiano na cuf au ZNP iliongozwa na Ali Mohsin Albarwan, baba yake mansour brigedia Yussuf Himid kama ungetokea muujiza wa kufuka leo angeshangaa kumona kijana wake akishiriki katika njama za usaliti wa kutaka kufuta mapinduzi aliyoyapigania kwa nguvu zake na kujitolea  kwa nchi  yake kuleta ukombozi"alisema kaimu huyo katibu mkuu .


Shaka alimtaka Mansour asifikiri kama wazanzibari ni wajinga na hawajui israf na ufujaji alioufanya akiwa serikalini alipokabidhiwa dhamana ya uongozi na sasa ametajirika.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI