Monday, September 7, 2015

CHAMA CHA TPP CHAPIGWA MARUFUKU KUFANYA KAMPENI

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania kimetoa onyo kali kwa Chama cha Tanzania Peoples Part (TPP) kutoshiriki katika shughuli zozote za kisiasa zinazoendelea nchini. .

Kauli hiyo imekuja baada ya Chama hicho kuonekana kuendelea na shughuli za kisiasa wakati kilishafutiwa usajili wake

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa Tanzania, Sisty Nyahoza amesema chama hicho kilishafutiwa usajili tangu Machi 20, 2002, chama kikishafutiwa usajili wake hakitakiwi kufanya shughuli zozote za kisiasa.

Nyahoza amesema ameshangazwa sana na watu waliojitokeza na kujitambulisha kuwa ni viongozi wa chama hicho waliojitokeza katika vyombo vya habari na kuanza kunadi sera licha ya kuwa chama hicho kilifutwa.

“Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa sura ya 358 kifungu cha 7(3) inakataza taasisi yoyote kufanya shughuli za kisiasa bila kusajiliwa na msajili wa vyama vya siasa.


“Sheria ya vyama vya siasa kifungu cha nane(b) ambacho kinazuia mtu yoyote kufanya shughuli za kisiasa kwa jina la chama ambacho yeye sio mwanachama wala kiongozi,” amesema Nyahoza ambaye aliongea kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI