MUIGIZAJI wa muda mrefu katika tasnia ya filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ yuko katika siku za mwisho za kuhitimisha harakati za kufunga ndoa, huku akijiapiza kuwa, endapo ataachika tena, basi atakuwa na nuksi.
Akipiga stori na paparazi wetu juzi, mmoja wa marafiki wa muda mrefu na Nora, ambaye pia ni msanii wa filamu (jina lipo kwenye droo zetu), alisema kwa sasa Nora yuko ‘bize’ kuhakikisha mambo na mipango ya harusi yake na mwanaume ambaye alitajwa kwa jina moja la Omary inakwenda sawa.
Katika kujua ukweli wa habari hiyo, Nora alitafutwa na alipopatikana alikuwa na haya ya kusema: “Jamani, kwani kuolewa ni kitu cha ajabu, ni kweli niko kwenye maandalizi hayo na ikitokea nimeachika tena, basi itabidi nijiangalie upya, ila naamini huyu wa sasa ndiye niliyekuwa namhitaji.”
0 comments:
Post a Comment