Monday, August 17, 2015

NAIBU WAZARI WA MAJI ATEMBELEA MAMLAKA YA MAJI MWANZA

NAIBU waziri wa maji Amos Makalla ametembelea Mamlaka ya maji jiji la Mwanza kwa kutembelea chanzo cha maji, kituo cha kutibu maji, ujenzi wa jengo la ofisi za mamlaka, mfumo wa majitaka na mkutano wa bodi na wafanyakaziKatika mkutano na bodi na wafanyakazi amewataka kutoa  huduma kwa wateja kwa kiwango cha juu ikiwemo kusikiliza matatizo ya wateja na kuyashughulikia kwa wakati.

Aidha ameitaka menejimenti kuhakikisha mkandarasi wa kujenga mradi mkubwa wa kuboresha huduma ya maji jiji la Mwanza hususan maeneo ya miinuko ananza kazi novemba kama ilivyopangwa.

Mradi huo mkubwa unagharimu shilingi bilioni 110 na ni ushirikiano wa serikali ya Tanzania. Shirika la maendeleo la Ulaya na ufaransa Kukamilika kwa mradi huu kutamaliza tatizo la maji jiji la Mwanza.
Bi Mary Matunge mtalaam wa urekebishaji mita akimweleza jambo naibu waziri wa maji.
Naibu waziri maji akipokea maelezo kutoka kwa mhandisi Davis Fute kuhusu majitaka.
Naibu waziri maji akihutubia bodi na watumishi. 
Mhandisi Stanley Mwasawale akimweleza naibu waziri wa Maji ujenzi wa jengo la mamlaka ya maji mwanza litakalogharimu shilingi bilioni 3.6

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI