Saturday, August 15, 2015

MZAMIAJI ALIFIKA SWEDEN SALAMA KABISA, LAKINI NDOTO YAKE IKAISHIA HAPOHAPO UWANJA WA NDEGE..!

follow-your-dreams-and-aspirations
JAMAA mmoja alijiandalia mazingira poa kabisa ya kuzamia kwenye ndege toka Ethiopia mpaka Sweden… alifika salama lakini hiyo bahati ya kuingia mitaa ya Sweden na kuanza maisha haikuwa upande wake, alinaswa mapema mapema baada ya ndege kutua Uwanja wa Ndege Arlanda, uliopo Sweden.
Jamaa alikamatwa na kukabidhiwa mikononi mwa Askari, alikutwa akiwa amejificha kwenye sehemu ya kuweka mizigo kwenye ndege hiyo ya Ethiopia Airlines, japo sehemu hiyo inakuwa na baridi kali sana lakini wakati ndege ikiwa safarini lakini kinachoshangaza ni kwamba jamaa kakutwa yuko sawa kabisa hana tatizo lolote kiafya.
“Wafanyakazi walipokuwa wanashusha mizigo walimkuta huyo mtu, yuko sawa kabisa ila tumemkabidhi wakamcheki afya yake pia”—hiki ndio alichokisema Henrik Klefve, Msemaji wa Kampuni ya Swedavia inayosimamia shughuli za Uwanja huo wa Ndege.
_84885000_swedethiopafpbody
Ofisa wa Polisi Anders Faerdigs amesema haya pia kuhusu mtu huyo >>>>
“Amesema alikuwa anafanya kazi Uwanja wa Ndege Addis Ababa, na tumemkuta na kitambulisho chake pia.. ndio maana aliweza kuingia na kujificha ndani ya ndege kirahisi”
Kingine ni kwamba wanahisi alijificha sehemu ya mizigo ambako huwa wanasafirishwa wanyama ambako kidogo kuna joto la kawaida kuliko sehemu ya mizigo ambayo ina baridi kali sana.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI