Mgombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia
cha cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinachoungwa mkono na vyama
vinne vinavyounda UKAWA kutoka Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward
Lowassa amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kugombea Urais katika uchaguzi utakao fanyika Oktoba 25, 2015.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva ndie aliyepokea fomu hizo na
kutangaza rasmi kumteua Edward Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Haji
Duni kuwania nafasi hizo kupitia vyama vyao.
Mwenyekiti wa Tume akisaini fomu hizo
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva akizungumza.
Lowassa akitoka ofisi za NEC huku akisindikizwa na viongozi wa UKAWA
Lowassa akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kurejesha fomu
Mheshimiwa Edward Lowassa akiongozana na Mgombea Mwenza Mh Juma Duni
Hajji na mkewe mama Regina Lowassa wakati wa kurudisha fomu kwenye ofisi
ya tume ya uchaguzi
Maalim Seif Shariff Hamad ni miongoni mwa viongozi wa UKAWA
waliomsindikiza Ndugu Edward Lowassa wakati anarudisha fomu ya kugombea
Urais
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akielekea kwenye ofisi za Tume
ya Uchaguzi wakati Ndugu Edward Lowassa akirudisha Fomu ya Kugombea
Urais kwenye ofisi za tume ya Taifa ya Uchaguzi.
(August 21, 2015)
#CHADEMA Blog
(August 21, 2015)
#CHADEMA Blog
0 comments:
Post a Comment