Thursday, August 27, 2015

ALIYEKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MASHA AACHIWA KWA DHAMANA

Lawrence Masha akiwa na wanachama wa Ukawa baada ya kuachiwa.
Baada ya jana kulala mahabusu ya segerea, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Masha, ambaye anashitakiwa kwa kosa la kuwazuia Polisi wasifanye kazi ikiwa ni pamoja na kuwatolea lugha ya matusi.
Alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo alisomewa mashtaka ambayo aliyakana lakini ikalazimu apelekwe mahabusu ya Segerea baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI