Thursday, March 19, 2015

MAJAJI WATATU WAFUKUZWA KAZI BAADA YA KUKUTWA WAKIANGALIA FILAMU ZA NGONO KWENYE KOMPYUTA ZA MAHAKAMA

Majaji watatu wamefutwa kazi kwa kutumia muda wao afisini kutizama filamu za ngono.
Jaji Timothy Bowles anayesikiza kesi za wilaya , jaji wa maswala ya uhamiaji Warren Grant na jaji Peter Bullock wamefutwa kazi.
Majaji hao walipatikana na hatia ya kutumia mtandao rasmi wa mahakama kwa mujibu wa wachunguzi wa idara ya mahakama.
Maafisa hao wanasemekana kuwa walitazama mitandao yenye filamu za ngono huku wakifahamu vyema kuwa ilikuwa ni ukiukaji wa sheria za matumizi kwa mujibu wa msimamizi wa idara hiyo ya Mahakama.
Hata hivyo kiongozi wa idara ya mahakama hiyo ya Uingereza na jaji mkuu waliwapata na hatia ya kwenda kinyume cha maadili ya mahakama.
Jaji wa nne Andrew Maw aliamua kustaafu mwenyewe wakati uchunguzi huo ukiendelea badala ya kufikishwa kizimbani.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya kisheria Clive Coleman kuwa makosa hayo yalikuwa makubwa sana katika mizani ya uadilifu wa majaji.
Aidha hakuna hata mmoja wao atakayeruhusiwa kufanya kazi katika idara ya mahakama tena.
#BBC

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI