Friday, January 9, 2015

YAYA TOURE AWEKA REKODI YA KUTWAA TUZO YA NNE MFULULIZO

yaya-toure

Bertha Lumala na mitandao
KUNGO wa Ivory Coast na Manchester City, Yaya Toure ametawazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika wa Shirikisho l;a Soka barani Afrika (CAF) kwa mwaka wa nne mfululizo.
Kiungo huyo ametwaa tena taji huilo baada ya kumbwaga  Mnigeria Vincent Enyeama, ambaye alionekana kuwa tishio kwake mwaka huu.
Hata hivyo, taifa lililong’ara zaidi usiku huu wakati wa kutunuku tuzo hizo, ni la Ukanda wa Kaskazini mwa Afrika, Algeria.
Timu ya Taifa hilo imetangazwa kuwa Timu Bora ya Mwaka, Klabu ya ES Setif Algeria imetangazwa kuwa Klabu Bora ya Mwaka na kocha swao mkuu, Kheireddine Madoui ametawazwa Kocha Bora wa Mwaka.
Katika kung’arisha zaidi tuzo hizo, Kinda wa Algeria, Yacine Brahimi ametangazwa kuwa ndiye Kinda Mwenye Kipaji Zaidi wa Mwaka Anayechipikia.
Wanawake wa Nigeria nao hawakuachwa nyuma wakati Falcons hao wakitangazwa Timu Bora ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka na Asisat Oshoala akaongeza tuzo nyingine kwa kuibuka Mchezaji Bora Kinda wa Mwaka na Mwanasoka Borav wa Kike wa Mwaka barani.
Tuzo ya Refa Bora wa Mwaka imekwenda kwa Papa Bakary Gassama, wakati Tuzo Mwanasoka Bora wa Mwaka anayecheza ndani ya Afrika imekwenda kwa Firmin Ndombe Makala

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI