Sunday, January 4, 2015

WAHI NAFASI YA KAZI HAPA: MHUDUMU WA OFISI II (OFFICE ASSISTANT II ) NAFASI - 10

44.0 MHUDUMU WA OFISI II (OFFICE ASSISTANT II ) NAFASI -10 
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Wahudumu hawa watafanyakazi za uhudumu katika ofisi ya Mkuu wa chuo katika vyuo vya maendeleo ya wananchi

44.1 MAJUKUMU YA KAZI 
• Kufungua na kufunga milango ya ofisi 
• Kufanya usafi wa ofisi. 
• Kupeleka vifurushi na barua 
• Kuhudumia miradi ya mafunzo chuoni. 

44.2 SIFA ZA MWOMBAJI 
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofaulu vizuri katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.

44.3 MSHAHARA 
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGOS A kwa mwezi

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i.       Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii.       Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii.      Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv.       Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v.       Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed C.V)  yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi.    Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
-       Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
-       Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-       Computer Certificate
-       Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) 
-       Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma. 
vii.       Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. 
viii.       Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix.       Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.       Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi.       Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii.       Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 18 Januari, 2015
xiii.      Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv.       Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Katibu,
Sekretariati ya Ajira katika
Utumishi wa Umma,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

AU

Secretary,
Public Service Recruitment
Secretariat,
SLP.63100,
Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI