Friday, January 2, 2015

SANDRA: SHILOLE USIDANGANYIKE NA PETE YA UCHUMBA

STAA  wa filamu Bongo, Salama Salmini ‘Sandra’ amemshauri msanii mwenzake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kupigania kuolewa na mwandani wake, Nuhu Mziwanda ambaye alimvisha pete ya uchumba siku chache zilizopita kwa kuwa kitendo hicho kwa sasa kimeshazoeleka.
Akiongea na mwandishi wetu, Sandra alisema anafagilia sana mapenzi ya wawili hao kwani anaona wanaendana pamoja na utofauti wa umri uliopo anamtaka Shilole ahakikishe anaolewa haraka iwezekanavyo kwani hata mwanadada Wema Sepetu alivishwa  pete ya uchumba na  Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ lakini mpaka sasa hawajafunga ndoa malengo yao yameishia njiani.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI