WAKATI Haiti ikisherehekea uhuru wake imekumbwa na maandamano ya wananchi katika maeneo mbalimbali wakishinikiza Rais wa nchi hiyo Michael Martelly kujiuzuru.
Baadhi ya maafisa ambao hawakutaka majina yao kutajwa wamesema makubaliano hayo yalitiwa saini Usiku wa kuamkia siku ya jumatatu kati ya Rais Michael Martelly na Marais wawili wa bunge na kusogeza mbele mamlaka ya bunge hadi mwezi april mwaka huu.
Mamlaka ya bunge ilipangwa kumaliza muda wake January 12 ambapo inge muacha Rais Michael Martelly akimaliza muda wake wa kuongoza nchi hiyo, matarajio ambayo yamesababisha maandamano ya upinzani katika taifa hilo maskini la Caribbean katika wiki za hivi karibuni.
Maafikiano hayo yamefikiwa na Rais, Mahakama, na Bunge huku Rais Martelly akiwataka watunga sheria kupitisha hatua hiyo kabla ya january 12.
Rais Michael Martelly
Rais huyo amemtaka waziri mkuu mpya Evans Paul kuunda serikali ambayo itakuwa na uwezo wa kupata imani kutoka kwa wana siasa wote lakini pia ikubalike na watu wote watakao shiriki katika uchaguzi.
Haiti imekuwa katika mgogoro wa kisiasa kwa miaka mitatu kufuatia kushindwa kwake katika kuandaa uchaguzi wa manispaa na sheria.
Aliyekuwa waziri mkuu Laurent Lamonthe Alijiuzuru mwezi huu kufuatia shinikizo la mara kwa mara dhidi yake kuachia ngazi kufuatia misuguano ya kisiasa.
0 comments:
Post a Comment