Thursday, January 8, 2015

POLISI WAANZA KUWASAKA WAHUSIKA MAUAJI YA WATU 12, UFARANSA *PICHAZ*

POLISI wa kupambana na ugaidi wa Ufaransa wameanzisha operesheni ya kuwasaka washambuliaji waliowaua watu 12 katika ofisi za jarida la kila wiki la Chalie Hebdo mjini Paris jana.
Televisheni za Ufaransa zimewaonyesha walenga shabaha wa kikosi maalumu cha polisi wakiwa katika barabara za mji wa Reims.
Washukiwa Said Kouachi na kaka yake Cherif.
Duru zilizo karibu na operesheni hiyo zikisema wanaume watatu, wawili kati yao wakiwa ndugu, Said Kouachi 32 na kaka yake Cherif 34 wame tambuliwa kama washukiwa. Ambapo mapema leo Polisi wametoa picha za ndugu hao.
Mmoja wa washukiwa hao watatu alifungwa jela mwaka 2008 kwa kuhusika na mtandao unao wapeleka wapiganaji nchini Iraq.
Vyombo vya Habari vya Ufaransa vimesema kijana mdogo mwenye umri wa miaka 18 ambaye amegunduliwa pia kama mshukiwa wa tatu Hamyd Mourad alijisalimisha polisi baada ya kuona jila lake katika mitandao ya kijamii.
Baadhi ya rafiki zake walisema katika mitandao hiyo kwamba alikuwa shule wakati shambulio hilo linafanyika katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo ambako watu 12 waliuawa.
Rais wa Ufaransa Francoise Hollande amelieleza shambulizi hilo kuwa la kigaidi na kutangaza leo kuwa siku ya maombolezo ya kitaifa.
Vyombo vya habari na viongozi mbalimbali ulimwenguni wamelilaani shambulizi la risasi dhidi ya wafanyakazi wa jarida la Charlie Hebdo mjini Paris, Ufaransa. Ambapo magazeti katika nchi mbalimbali yalishamiri na taarifa hiyo.
Katika mitaa mbali mbali, Zaidi ya watu laki moja walionekana kutanda katika baadhi ya mitaa nchini ufaransa ikiwa ni hatua ya kuelezea hasisa zao huku wakiwa wamebeba mabango mbalimbali yanayopingana na kitendo hicho.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI