Wednesday, January 21, 2015

MTAZAME MAMBA ALIYEKULA WATU HUKO SENGEREMA *PICHAZ*

Mzoga wa mamba mmoja ukiwa umezungukwa na wanakijiji wa Kome-Mchangani.
Mzoga wa mamba mwingine.
Mzee aliyewatega mamba hao (aliyeketi) akiwa nyuma ya mzoga wa mamba mmojawapo.
Mwanakijiji akiweka pozi juu ya mzoga wa mamba kuonesha furaha yake.
*********
WANAKIJIJI wa Kome-Mchangani wilayani Sengerema mkoani Mwanza, wamewaua mamba wawili wanaodaiwa kuua watu wawili na kuwajeruhi watu watatu.Mamba hao waliokuwa katikakingo za Ziwa Victoria kijijini hapo, walitajwa kuwa kero kubwa kiasi cha kusababisha baadhi ya shughuli za kuinua uchumi katika kijiji hicho kama vile uvuvi na umwagiliaji kusimama kwa muda huku wanakijiji wakiwa na hofu ya kuliwa na mamba hao.Wakizungumza na mwandishi wetu, wanakijiji hao walidai kuwa mara kadhaa walifikisha malalamiko yao kwa viongozi wa serikali lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, jambo lililowafanya wachange pesa na kumpa mzee mmoja ambaye alitumia mbinu za kitaalamu kuwatega mamba hao na hatimaye kuwaua.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI