Diwani wa kata ya Kibindu Mawazo Mkufya aliyenyanyua mikono juu akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kulia aliyevaa kofia ya kijani kufuatia mvua kubwa kubomoa madarasa ya shule ya Msingi Kibindu.
Moja ya darasa la shule ya msingi Kibindu likiwa limebomoka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa mwaka jana.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa Habari mbele ya jengo la shule ya Msingi Kibindu ambalo lilianguka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa mwaka jana kushoto ni diwani wa kata ya Kibindu Mawazo Mkufya.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa Kata ya Kibindu alipofika kuwajulia hali kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa mwaka jana.
*********
WANAFUNZI wa shule ya Msingi Kibindu wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wako hatarini kuangukiwa na vyumba vya madarasa wanayosomea kutokana na ubovu wa vyumba hivyo ambavyo vimejengwa miaka ya 50.
Mwishoni mwa mwaka jana vyumba vya madarasa mawili na ofisi ya mwalimu vilianguka na kuezua mapaa ya vyumba vine vya madarasa na ofisi ya mwalimu mkuu baada ya kutokea mvua kubwa amabyo iliambatana na kimbunga.
Shule hiyo ambayo ina wanafunzi 970 hawakuwepo shuleni kwani walikuwa wako likizo ya mwisho wa mwaka baada ya shule kufungwa mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye alitembelea shuel hiyo ofisa mtendaji wa kijiji cha kibindu Juma Athuman alisema kuwa mvua hiyo kubwa iliambatana na kimbunga ilinyesha Desemba 28 mwaka jana na kuangusha majengo mawili ya madarasa pamojana na kueezua mapaa ya vyumba vinne vya madasa na na ofisi ya mwalimu mkuu.
Athuman alisema kuwa kimunga hicho pia kilisababisha ufa katika majengo mengine kadhaa ya madarasa katika shule hiyo na kuwa katika hatari kubwa ya kuanguka.
“Hali hiyo inatia wasiwasi kwa wanafunzi wnaotarajiwa kuanza masomo Januari 14 mwezi huu kuwa hatarini kuangukiwa na majengo hayo endapo hatua za dharura hazitachukuliwa,” alisema Athuman.
Akizungumzia mara baada ya kutembelea shule hiyo Mbunge wa Jimbo la Chalizne Ridhiwani Kikwete amesikitishwa na hali hiyo ya majengo ya shule hiyo na kusema kuwa anafanya taratibu za kuwasiliana na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kuona jinsi ya kujenga upya shule hiyo.
0 comments:
Post a Comment