VIJANA watatu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, wamekamatwa na polisi eneo la Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 2, 2014, baada ya jaribio lao la kufanya matembezi kutoka mkoa wa Geita wakielekea Ikulu ya Dar es Salaam kumuona Rais Jakaya Kikwete kufikisha malalamiko yao.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, vijana hao watatu, Juma Maganga, Khalifa Selemani na Athanas Michael, walielekezwa na maafisa usalama kumuona yeye DC baada ya kuwasili kwenye eneo lake la utawala wakitokea Geita, ili awape baraka za kwenda Ikulu. Lakini walipofika ofisini hapo, DC huyo alitaka kujua nini hasa kilichowafanya watembee safari ndefu kama hiyo?
DC Rugimbana alisema, walimweleza kuwa Mosi, Wanataka Kumnuona Rais ili wamueleze kuchukizwa kwao na vitendo vya viongozi kula rushwa na hakuna hatua dhabiti zinazochukuliwa dhidi yao, kukithiri kw amatumizi mabaya ya rasilimali za taifa, kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia, na kudai kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika.
Baada ya kusikia hayo, DC aliwaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kumuona Rais wa nchi, hata hivyo sio kumuona kiholela bali ni kwa utaratibu maalum, na kwa kufikia hatua waliyofikia vijana hao, tayari walikuwa wamevunja sheria lakini akawataka wasubiri awasiliane na wakubwa ili waandaliwe utaratibu wa kumuona Rais.
Hata hivyo vijana hao walikataa na walipotoka nje ya ofisi ya DC hapo Kinondoni, walifanya tena jaribio la kuelekea Ikulu na safari hii polisi hawakufanya masihara, waliwaweka chini ya ulinzi mita chache kutoka taa za kuongozea magari kwenye makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa ukiwa uneelekea Kariakoo.
Vijana hao wakiwa kwenye safari yao eneo la Magomeni Kagera
Vijana hao wakiwa chini ya ulinzi wa polisi wakielekea kituo cha polisi Magomeni Mapipa
Polisi wa kutuliza ghasia akiwahi sehemu walikoelekea vijana hao tayari kuwakamata
Polisi wakionye raia kutounga "tela" safari ya vijana hao wakati wakiwa eleo la Magomeni Mwembechai
Polisi wakimdhibiti mmoja w avijana wasiokubali "kupitwa"
Polisi wakiwahi kukamata vijana
Vijana wakiwa chini ya ulinzi
Wakionyesha mshikamano baada ya kukamatwa.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, akiwaeleza waandishi wa habari matokeo ya mazungumzo yake na vijana hao.
0 comments:
Post a Comment