Sunday, January 4, 2015

MAKUBWA TENA...SUPU YA PWEZA KIGEU GEU, SASA YAMALIZA NGUVU ZA KIUME NA SI KUZIONGEZA

Yale maelezo kuwa supu ya Pweza na dawa za mitishamba zinazotolewa na ‘Sangoma’ zinaongeza nguvu za kiume huenda yakawa si kweli baada ya kuwepo taarifa kuwa dawa hizo zinapunguza kama si kumaliza kabisa nguvu hizo.

Baadhi ya wateja na jamaa wanaotumia dawa hizo wamesema baadhi ya ndugu zao waliotumia dawa hizo wameshidwa kufanya tendo la ndoa.

Walisema wakati mwingine walivyoanza kuzitumia walipata uwezo wa kindoa lakini hali ilibadilika na nguvu ziliishi na sasa wanajuta kutumia dawa hizo.

Walidai kuwa waganga wa jadi na wapishi wa supu ya pweza wanawahadaa kuwa wanadawa lakini wanachotumia ni kuchanganya dawa zao na viagra.
Walisema kuna baadhi ya hotel na migahawa inasifika kwa kutengeneza dawa hizo zinazowavutia wateja na kushawishika kufunga safari kwenda kuzinunua lakini kinachoongezewa ni kusisimua misuli ya viungo ni tiba za kisasa na vingine vyote ni viini macho.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI