MAGARI yote yenye namba za usajili za Tanzania yanayofanya biashara ya kusafirisha abiria ikiwemo watalii kutoka Arusha kwenda Nairobi nchini Kenya yamezuiliwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Hatua ya kuyazuia magari hayo ilianza kuchukuliwa tangu Disemba 28 mwaka jana na mamlaka ya Serikali ya Kenya bila kueleza hasa Sababu za kuyazuia hayo kuingia uwanjani kama ilivyokua zamani.
Mmiliki wa kampuni ya Rainbow Shuttle Methew Molel alisema kitendo cha kuyazuia magari hayo na kusababisha kulipa gharama mara mbili ni hujuma kwa biashara yao.
“Tumesikitishwa na kitendo cha kuyazuia magari yetu umbali wa kilomita mbili hadi tatu kutoka uwanjani,ambapo tunalazimika kulipia tena ushuru kwa gharama ya dola 10 hadi 12 za Marekani kwa mgeni ,fedha ambayo ni karibu 22,000kwa fedha ya Kitanzania,hii ni hujuma kwa uchumi wa nchi yetu na ni dalili mbaya kwa mtangamano wa Jumuiya ya EAC”Alisema Mollel.
0 comments:
Post a Comment