Wednesday, January 21, 2015

ARSENAL WAMSAJILI KIUNGO KUTOKA POLAND

ARSENAL wamemasajili kiungo Krystian Bielik kutoka klabu ya Legia Warsaw ya Poland kwa pauni milioni 2.4. Bielik, 17, ambaye alifanya vipimo vya afya wiki iliyopita, alihamia Legia akitokea Lech Poznan mwaka jana na amecheza mara sita msimu huu. Arsenal wamesema mkataba huo "utakamilika baada ya mchakato wa kawaida kumalizika". Bielik, ambaye aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Poland ya chini ya miaka 16, anaweza kucheza kama kiungo wa kati, au beki wa kati.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI