Tuesday, December 30, 2014

UTAFITI: FURAHA IMEONGEZEKA DUNIANI...ETI HADI NCHI HII ILIYOTAWALIWA NA VITA INA FURAHA..!

8813468-happy-girl-wallpaper
UTAFITI uliofanyika katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka umegundua kuwa hali ya kuwa na furaha miongoni mwa watu mbalimbali duniani kwa jumla imeongezeka katika kipindi cha mwaka mmoja .
Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika kwenye nchi 65 ambao ulihusisha watu wapata 64,000 furaha itokanayo na sababu mbalimbali imeongezeka tofauti na hali ilivyokuwa mwanzoni mwa mwaka.
Utafiti huu umeoneysha kuwa angalau asilimia 70% ya watu katika mataifa ambayo yamehusika kwenye utafiti huu wameridhika na hali ya maisha yao jambo ambalo linaongeza furaha .
Taifa la Fiji ambalo liko kwenye bara la Oceani kusini mashariki mwa dunia limeonekana kuwa taifa linaloongoza kwa furaha kutokana na asilimia 93% ya raia wanaoishi kwenye taifa hilo kuridhika na maisha yao
Taifa la Fiji limetajwa kuwa taifa linaloongoza kwa furaha kwa mwaka 2014.
 Kinyume na Fiji taifa la Iraq limeonekana kuwa taifa linaloongoza kwa majonzi na furaha duni baada ya majibu ya utafiti kuonyesha kuwa taifa hilo lina asilimia 31% pekee ya watu wanaoridhishwa na maisha yao .
Katika hali isiyiokuwa ya kawaida bara la Afrika limetajwa kwenye utafiit huo kuwa bara linaloongoza kwa furaha ambapo asilimia 83 % ya wakazi wa bara hilo wamekiri kufurahishwa na maisha kwa jumla .
Eneo la ukanda wa magharibi mwa bara la ulaya limeonekana kuwa eneo ambalo watu wake hawana furaha kuliko maeneo yote kutokana na kuwa na asilimia 11% pekee ya watu ambao wamekiri kuwa na furaha maishani mwao.
Iraq imeonekana kuwa nchi yenye furaha kwa kiwango cha chini kuliko yote duniani.
 Katika utafiti huo asilimia 65% ya watu ulimwenguni kote walikuwa na maoni kuwa mwaka 2015 utakuwa mwaka mzuri kuliko mwaka 2014 baada ya robo tatu ya wakazi wa bara la Afrika na asilimia 26% ya wakazi wa magharibi mwa bara la ulaya wakiwa na uhakika juu ya kupata aina Fulani ya maendeleo katika mwaka ujao.
Utafiti huo pia umeitaja Nigeria kuwa nchi yenye hisia chanya kuliko mataifa yote huku Lebanon likiwa taifa linaloongoza kwa kuwa na hisia hasi kuliko yote.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI