Picha: Maktaba
Na Shija Felician, Kahama.
MAISHA ya wananchi wa kata ya mwendakulima wanaozunguka mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama mkoani Shinyanga yako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kunywa maji yenye mchanganyiko na kinyesi cha binadamu.
Hali hiyo imebainishwa kwenye mkutano wa hadhara wa kamati ya bunge Ardhi maliasili na mazingira ambao wananchi hao walihoji uhalali wa walinzi wa mgodi wa Buzwagi kumwaga maji safi yanayochotwa kwenye eneo linalomilikiwa na mgodi huo.
Katika mkutano huo wananchi hao wamedai maeneo ya visima vya kuchota maji yamebanwa na matumizi ya kibinadamu hali ambayo baadhi ya vinyesi vya binadamu hutiririka na kujichanganya kwenye maji hayo hali ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu.
Walisema kutokana na hali hiyo visima vyenye maji safi na salama viko kwenye eneo linalomilikiwa na mgodi wa Buzwagi lakini wananchi wakienda kuchota humo maji hayo humwagwa na walinzi wa mgodi huo.
Hata hivyo malalamiko hayo mwenyekiti wa kamati hiyo James Lembeli amemtaka naibu waziri wa bunge Ardhi maliasili na mazingira Ummy Mwalimu kulitolea ufafanuzi lalamiko hilo kwa kuwa suala la uchafuzi wa maji liko kwenye wizara yake
Kwa upande wake naibu waziri huyo aliyekuwa ameambatana na kamati hiyo kuzungukia migodi ya dhahabu amesema suala la ujenzi wa visima vya maji salama sio la mgodi bali ni la halimashauri yao ya mji ni suala la serikali ya kijiji kupeleka mipango kazi ya kujengewa visima.
Chanzo: Kijukuu Blog.
0 comments:
Post a Comment