WASIKILIZAJI wa kipindi cha ‘Genge’ cha 93.7 E-FM ya Dar es Salaam wamepokea kwa masikitiko taarifa kutoka kwa mtangazaji wa kipindi hicho waliyekuwa wamemzoea, Penniel Mungilwa a.k.a VJ Penny kuwa hatasikika tena kwenye kipindi hicho.
Kupitia Instagram Penny ameandika:
“Gengerzzz hata sijui nianzie wapi, ila wacha niwaambie nawaona nyie wote kama familia yangu…toka day 1 mmekua na bonge la support! Message zenu ndio zilikua zinatuunganisha kama tunajuana…sina cha kuwalipa! I love u all beyond words!
Sasa time yangu ya kufanya Genge imekwisha, ila sio ndio muondoke kimoja.. Mpeni support jamaa anaefuata, project zingine kali zinakuja ntawasanua, si mnajuanga napenda kuwapa vitu flani flani AMAZING??? I SALUTE ALL OF U…camp,unit, crew zote! Wadau wote mlitisha…kila jambo lina mwanzo na mwisho! Nimemaliza kazi yangu ya Genge..na wote mjipongeze kwa pamoja tulifanya vitu AMAZING…ALUTA CONTINUA! Baraka tele kwenu GENGERZ”
0 comments:
Post a Comment