Thursday, November 6, 2014

OBAMA AAHIDI KUFANYA KAZI NA UPINZANI KATIKA UTAWALA WAKE *PICHAZ*

RAIS wa Marekani Barack Obama na kiongozi wa wajumbe wa chama cha upinzani cha Republican walio wengi katika baraza la Seneti Mitch McConnell, wametoa ahadi ya kushirikiana kusaidia utendaji wa serikali na wameahidi kumaliza mvutano wa kisiasa ambao umewavunja moyo wapiga kura wa Marekani.
Wanachama wa Republican wamepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi wa nusu muhula na kwa sasa wanadhibiti mabunge yote mawili nchini Marekani.
Mitch McConnell
Kiongozi wa baraza la Senate anayeingia madarakani Mitch McConnell amesema ataliwezesha baraza hilo kufanya kazi na kupitisha miswada ya sheria. Pia ameahidi kufanyakazi pamoja na Obama katika masuala kama vile mikataba ya kibiashara na marekebisho ya kodi.

Rais Barack Obama amesema alikuwa na 
"hamu ya kufanyakazi na baraza jipya la Congress na kufanya miaka yake miwili aliyobaki kukaa madarakani kuwa na tija kadiri iwezekanavyo". 
Na amewaambia Wamarekani waliopiga kura ya kutaka mabadiliko kuwa "nimewasikia"

Obama pia amekiri kuwa  kama rais ana wajibu wa kipekee kujaribu kuona chombo hiki kinafanya kazi, na siku ya ijumaa ameandaa mkutano wa viongozi wa chama tawala cha Democratic na upinzani Republican akisisitiza kuwa wanaweza kufanya kazi pamoja. Na niwakati wa kushungulikia masuala ya manufaa kwa Umma.

Lakini rais Obama ameonya kuwa atachukua uamuzi binafsi kupunguza uondoaji wa wageni na kuimarisha usalama wa mipaka-hatua ambayo aliichelewesha hadi baada ya uchaguzi, kitu kilichowachukiza sana baadhi ya wapiga kura wa Amerika ya Kusini.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI