Sunday, November 2, 2014

MTOTO WA KIM KARDASHIAN NA KANYE 'NORTH WEST' AFUNIKA KATIKA HALLOWEEN NEW YORK 2014

WATU mbalimbali wamejitokeza katika mitaa ya jijini New York katika gwaride la mwaka kuadhimisha tamasha la 41 la kiutamaduni maarufu kama Halloween.
Sherehe hizo zinazo husisha uvaaji wa mavazi ya ajabu ikiwemo ya wanyama huadhimishwa na nchi mbalimbali kila inapofika October 31
Moja ya nchi inayoadhimisha siku hii ni pamoja na Marekani ambapo katika mitaa ya New York, Gwaride kubwa lilifanyika likiongozwa na bendi huku wapigaji bendi wakiwa na vinyago usoni.
Watu mbalimbali wamejitokeza kama wachezaji hawa, wakiwa na mavazi ya aina ya kipekee ambayo ndio kivutio kikubwa katika Tamasha hili.
Tazama kina dada hapa, wakicheza kwa madaha wakiwa na mavazi ya mdudu aina ya kipepeo na kuwa kivutio kikubwa kwa watazamaji wakiwemo watoto huku mshiriki huyu kinyago cha fuvu akijaribu kuwatisha mashabiki.
Sherehe hizi ambazo husherehekewa katika nchi mbalimbali za ulaya pia husheherekewa na watu maarufu kuvaa mavazi yenye sura mbalimba kama mtoto wa kanye west yaani North west alivyotokea katika vazi la Nyau, Tylor Swift, Caty Perry na wengine.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI