Saturday, November 1, 2014

MKANDALA AKANUSHA TAARIFA KUHUSU DIAMOND KUTUNIKIWA PHD NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandala amekanusha taarifa zilizozagaa zinazodai kuwa msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz atatunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) kutokana na mchango wake kwa jamii.
Akizungumza na Power Jams ya East Africa Radio, Prof. Rwekaza Mukandala ambae yupo nje ya nchi kwa sasa amesema taarifa hizo si za kweli ni uzushi tu.
“Hizi tetesi ni za uvumi, si za kweli,” alinukuliwa na mtangazaji wa radio hiyo ambapo alidai walishindwa kuelewana vizuri kutokana na mawasiliano kuwa si mazuri.
Hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii iliibuka taarifa iliyosema: 
Katika mahafali ya 44 ya Chuo Kikuu Dar es Salaam yatakayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City tarehe 08 November 2014, aliyekuwa mkuu wa chuo (Chancellor) wa UDSM marehemu Balozi Fulgence Kazaura na msanii maarufu Afrika aliyeshinda tunzo nyingi zaidi kuliko wasanii wote Tanzania Diamond Platinumz watatunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima (Honoris Causa) ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa mchango wao kwenye jamii.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI