Wednesday, November 5, 2014

MFAHAMU MWANAUME HUYU ALIYEPANIA KUIJAZA DUNIA KWA KUZAA WATOTO 50 *PICHAZ*

Halit Tekin akihojiwa na chombo kimoja cha habari nchini humo.
BWANA mmoja nchini Uturuki, ambaye ana watoto 32 kutoka kwa wake zake wanne amesema analenga kufikisha watoto 50.
Kuwa na mke zaidi ya mmoja nchini Uturuki ni kinyume cha sheria, lakini Halit Tekin, amefunga ndoa 'isivyo rasmi' na wanawake watatu, tangu alipomuoa mke wake wa kwanza rasmi mwaka 1982, imeripoti tovuti ya Hurriyet Daily News.
Bwana Halit Tekin akipozi katika picha na baadhi ya wanae na mkewe aliyetoka kujifungua hivi karibuni.
Bwana Tekin, 54, ambaye anaishi katika jimbo la Hatay, hivi karibuni alipata mtoto wa kiume na mke wake wa kwanza.
Mtoto huyo amempa jina a Ahmet. 
"Hii leo nina watoto 32, na 12 kati yao ni wa kiume. Nawapenda wote. Ikiwa afya yangu itaniruhusu, Mungu akipenda, nataka nifikishe watoto 50" amesema.
Wake zake hao wanaishi katika nyumba tofauti pamoja na watoto wao
"kwa sababu hatutoshi katika nyumba moja" amesema na kuongeza kuwa kuna "maelewano mazuri" miongoni mwao.
Licha ya kupigwa marufuku ndoa za wake wengi, uchunguzi uliofanywa mwaka 2013 na bunge la Uturuki ulibaini kuwa wanaume 372,000 wana ndoa ya zaidi ya mke mmoja, imeripoti tovuti hiyo.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mara kadhaa alikuwa akitaka familia kuwa na watoto japo watatu, wakati huo akiwa Waziri Mkuu, 'ili nchi iwe na nguvu'.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI