TUNAKULETEA idadi ya marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani.
ABRAHAM Lincoln; alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865 jijini Washington kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes. Alikuwa amekaa na mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer.
INDIRA Gandhi; alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New Delh, India.
JOHN Francis Kennedy ‘JFK’
Ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1963 mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la wazi barabarani.LAURENT Desire Kabila; alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa ni walinzi wake.
THOMAS Isdor Noel Sankara
Alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa kupigwa risasi na Blaise Compaore ambaye hivi karibuni ameikimbia nchi hiyo.
WILLIAM Richard Tolbert Jr
Alipigwa risasi mwaka 1980 katika mapinduzi ya kijeshi akiwa Rais wa Liberia. Samuel Doe akiwa na cheo cha sajenti ndiye aliyetajwa kumuua.
MUHAMMAR Muhamad Abu Migar al Ghaddaf
Alikuwa Rais wa Libya kwa miaka 42. Aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa kwenye vurugu za kisiasa mjini Sirte, Libya, Oktoba 20, 2011.
ABEID Amani Karume
Alikuwa Rais wa Zanzibar tangu mapinduzi ya mwaka 1964. Aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anacheza bao mwaka 1972 na mtu ambaye hakuwahi kupatikana.
Jean baptist ouedraogo
Aliitawala Burkina Faso kwa mwaka mmoja tu, 1982-83. Aliuawa kwa kupigwa risasi na Thomas Sankara ambaye alichukua madaraka ya kuiongoza nchi hiyo kabla na yeye kupinduliwa.
0 comments:
Post a Comment