Saturday, November 1, 2014

KULALA NA WANAWAKE WENGI KUNAPUNGUZA HATARI YA KUPATIKANA NA UGONJWA WA SARATANI YA KIBOFU CHA MKOJO

KULALA na wanawake wengi kunapunguza hatari ya kupatikana na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo,kulingana na utafiti.
Katika utafiti uliochapishwa katika jarida la saratani,Watafiti kutoka chuo kikuu cha Montreal wamebaini kwamba ikilinganishwa na wanaume walio na mpenzi mmoja katika maisha yao yote,kulala na zaidi ya wanawake 20 kunapunguza uwezekano wa kupatikana na ugonjwa huo kwa asilimia 28.
Wanaume 3,208 walishiriki katika utafiti huo ambapo kati yao Wanaume 1,590 walipatikana na ugonjwa huo kati ya Septemba mwaka 2005 na Agosti mwaka 2009.
Kwa jumla watafiti hao walibaini kwamba wanaume wenye saratani ya kibofu cha mkojo kuna uwezekano mara mbili kwa wao kuwa na watu wa familia zao wenye saratani.
Hatahivyo ushahidi unaonyesha kwamba idadi kubwa ya wapenzi wa kike miongoni mwa wanaume inapunguza tishio la ugonjwa huo.
Mwanamume anapojamiana na zaidi ya wanawake 20 katika maisha yake,tisho la kupata ugonjwa huo linapoungua kwa asilimia 28 mbali na asilimia 19 kwa aina yoyote ya ugonjwa wa saratani.
Utafiti huo pia umebaini kwamba mmoja kati ya wanaume wanne wa kiafrika hupatikana na saratani

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI