FILAMU ya Wape Salamu Zao itazinduliwa Jumapili ya tarehe 9 November katika ukumbi Travetine Magomeni, jijini Dar es salaam.
Uzinduzi huo utambatana na ujio wa msimu wa 2 wa kipindi cha Ulimwenguni wa filamu cha TBC 1, Mkinachoongozwa na Juma Mtetwa katika.
Aidha kutakuwa na vivutio vya kukata na shoka akiwemo mheshimiwa Jackson Kabirigi ‘Kisate’.
Akizungumza Kisate alisema:
“Nimepanga kuacha historia katika uzinduzi wa filamu ya Wape Salamu Zao, kuna vitu vingi sana ambavyo sijawahi kuwaonyesha watazamaji hajawahi kuviona kutoka kwangu tarajieni maajabu.”
Aidha gwiji la muziki wa Taarab Bongo mfalme Mzee Yusuf atakuwepo.
Kiingilio katika hafla hiyo ambayo pia itawakutanisha Wasanii nyota wa filamu kutoka Bongo movie ndani ya zuria jekundu ni 8,000/ tu kwa mtu mmoja.
0 comments:
Post a Comment