Thursday, November 20, 2014

DOKII WA BONGO MOVIE ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE 2015, SOMA HAPA KUJUA NI JIMBO LIPI?

2015 ndio imekaribia na tayari mpaka sasa tumeshasikia wengi tu wakitangaza au kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya uongozi kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania zikiwemo nafasi za Urais na Ubunge.
Mwigizaji wa longtime kwenye game ya Tanzania ambaye alianzia kwenye maigizo Tanzania amechukua nafasi kwenye Amplifaya ya CloudsFM inayosikika J3-Ijumaa saa moja jioni na kusema anayo nia ya kugombea Ubunge 2015 Kilosa Morogoro.
‘Nagombea Ubunge katika jimbo la Kilosa, naomba tu Neema ya Mungu iniongoze kwa sababu kila kitu huwa nafanya na kusikiliza nini Mungu anaongea na mimi, nia yangu ni kugombea Kilosa sababu ndio nimetokea huko japo mimi ni mtu wa Kigoma Mmanyema lakini nimekulia kule Kilosa Kimamba Morogoro‘ – Dokii

‘Mimi ni msanii pekee naweza kusema ndio nimetumika sana kwenye jamii kuliko wasanii wote, kwenye kuelimisha jamii najitolea hata kipindi kile cha madereva wa bodaboda mpaka wakanipa Ubalozi nilikua nakaa natetea haki zao, na pia nataka kuonyesha kwamba Wanawake tunaweza hapana kujiweka nyuma‘ kamalizia Dokii

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI