SHUGHULI za viwanda nchini China zimeshuka kwa mwezi wa tano mfululuzo kinyume na matarajio ya nchi hiyo.
kushuka huko kumesababishwa na uagizaji mdogo wa bidhaa na kupanda kwa Gharama za uzalishaji viwandani.
Taarifa kutoka ofisi ya ununuzi zinasema kuwa shuguhli hizo zimepungua kwa mwezi October na kufikia asilimia 50.8 kutoka asilimia 51.1 ya mwezi September kinyume na matarajio ya wachambuzi wa uchumi ya kiasi cha asilimia 51.2 kilicho tegemewa.
Ofisi ya ununuzi imeonesha kuwa mahitaji ya ndani na nje ya nchi yameshuka kwa muda wa miezi sita mfululizo huku uagizaji wa bidhaa Ukionekana kushuka kila mwezi.
Taarifa hiyo inabainisha kuwa hesabu za bidhaa ambazo hazi jauzwa imeongezeka mwezi uliopita pamoja na kwamba viwanda nchini humo vime punguza kiwango cha uzalishaji.
Wachambuzi pamoja na benki ya uwekezaji nchini humo wanasema kuwa, hii ni dalili kuwa China bado inakabiliwa na changamoto katika ukuaji wa uchumi ikiwa ni nchi ya pili yenye uchumi mkubwa duniani.
0 comments:
Post a Comment