Saturday, October 18, 2014

SIMBA NA YANGA ZASHINDWA KUWAPA MASHABIKI WAKE KITU ROHO INAPENDA KWA KUTOKA NUNGE, BILA KUFUNGANA

NB: Picha hii si ya tukio la leo.
MIAMBA ya soka simba na yanga imegawana pointi baada ya kutoa sare ya bila kufungana jioni hii katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo kipa chipukizi Peter Manyika wa timu ya Simba aliibuka shujaa kwa kuokoa michomo kadhaa ya Hatari.
Kipa huyo alidaka mechi hiyo ya watani wa jadi leo kwa kuwa kipa wa kwanza Ivo Mapunda na wa pili Hussein Sharrif wote wakiwa majeruhi na watani wao Yanga wakiamini itakuwa ni njia rahisi kwao kujipatia ushindi

Lakini mpaka kunako dakika ya tisini ya mchezo hakuna Mbabe kati ya Simba wala Yanga.
Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kuwa kileleni kwa kuwa na Point 7 huku mshindani wake Simba aliyeingia akiwa na Point 3 sasa ameambulia point 1 hivyo kuwa na point 4 kibindoni.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI