Roberto Di Matteo
ALIYEKUWA
meneja wa Chelsea na Wesbromwich Albion kwa nyakati tofauti, Roberto Di
Matteo sasa ameramba shavu lingine nchini Ujerumani baada ya
klabu ya Schalke 04 kumtangaza kuwa meneja mpya wa klabu hiyo.
Di
Matteo, mwenye asili ya nchini Italy, amejiunga na Schalke baada ya
aliye kuwa kocha wa timu hiyo, Jens Keller kufungashiwa virago kwa
sababu ya matoke mabavu yanayo iandama klbub hiyo tanga ligi kuu nchi
Ujermani msimu wa 2014/2015 ianze.
Schalke
ipo katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Bundesliga wakiwa
wamejikusanyia jumla ya pointi nane tu kutoka michezo saba walizocheza
ambapo pia wamefanikiwa kushinda mechi mbili pekee kati hizo.
Lakini
katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, Schalke ipo katika
nafasi ya tatu katika kundi lao baada ya kutoa sare kwenye mechi mbili
alizozicheza mpaka sasa ambopo moja kati ya hizo mechi ni ile dhidi ya
Chelsea ambayo walitoka sare ya 1-1 dimbani Stanford Bridge.
Kati ya
mechi ngumu ambayo Schalke 04 inategemea kucheza ikiwa chini ya Di
Matteo ni mchezo ujao wa Novemba 25 dhi ya Chelsea ( klabu bingwa
barani Ulaya).
0 comments:
Post a Comment